Eeh Mungu baba wa taifa la leo Tunayekuabudu umetuachia kilio, lio Siwezi sema nikisema sana nitakufuru (Mi nitakufuru)
Hata maandiko yanasema we ni zaidi ya nuru
Na unalolipanga hakuna wa kupangua Yoyote umtakae Baba we unamchukua Inaniuma sana nikikumbuka babu Magu Mi nawaza sana nakosa majibu, jibu
Mi nikitazama sana fly over za juu kwa juu Usemi wa mama rais Magu ana viwango vya juu
Leo hatunaye tena, baba baba, babaa Rais Magufuli, baba baba baba Mtetezi wa wanyonge baba baba Umetuachia kilio, baba baba Daima tutakukumbuka
Kaza moyo Janet Magufuli nakupa pole Mama Samia Suluhu
Kaza moyo funga mkanda, ujikaze nganga nganganga Kupeperusha bendera ya Tanzania
Hivi ni nani atakayeziba pengo la babu Hivi ni nani ziba pengo sioni Na dua tunakuombea, pumzika salama Na dua tunakuombea, pumzika salama babu Na dua tunakuombea Na dua tunakuombea, pumzika salama Magu