Accueil  đŸ’ƒđŸŽ€ Paroles de chanson Française et Internationnales

 A   B   C   D   E   F   G   H   I   J   K   L   M   N   O   P   Q   R   S   T   U   V   W   X   Y   Z   0   1   2   3   4   5   6   7   8   9 
Artiste : Akothee
Titre : Baraka
Kwangu imekuwa kama ndoto au nyota
Iliojaa upendo usio na kipimo
Na umeniinua leo naitwa mama kijacho
Naisubiri zawadi kutoka kwako

Maombi yangu usiku na mchana
Aje mtoto mwenye hekima na busara
Mkarimu na mcheshi na asiwe hasara

Mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu
Nitamlea kwa nguvu za Mungu
Umenipa dhamani mbele za macho ya watu
Acha niringe nitambe na nipige nduru

Acha niringe, nitambe na nipige nduru
Acha niringe, nitambe na nipige nduru

Kwani mimi ni nani
Unichague niwe mama wa watoto wako
Asante, kwa kukubali niwe wako

Kwani mimi, ni nani?
Unikubali niwe mama wa watoto wako

Kwani mimi ni nani
Unichague niwe baba wa watoto wako
Asante, kwa kukubali niwe wako

Kwani mimi, ni nani?
Unikubali niwe baba wa watoto wako

Umenitendea haki aliyonipa mama
Umenionyesha upendo sijawahi ona
Nayainua macho yangu juu
Nikualikie mema kutoka kwa Mungu

Tulipo ianza safari
Kunawaliopinga na kutukatisha tamaa
Hukuvunjika moyo ata maisha yalipokwenda mrama

Mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu

Nitamlea kwa nguvu za Mungu

Acha niringe, nitambe na nipige nduru
Acha niringe, nitambe na nipige nduru

Kwani mimi ni nani
Unichague niwe mama wa watoto wako
Asante, kukubali niwe wako

Kwani mimi ni nani
Unichague niwe mama wa watoto wako
Asante, kwa kukubali niwe wako

Kwani mimi ni nani
Unichague niwe baba wa watoto wako
Asante, kwa kukubali niwe wako

Kwani mimi, ni nani?

Unikubali niwe baba wa watoto wako

Kwani mimi, ni nani?
Unikubali niwe mama wa watoto wako