Pale mambo yanapoonekana hayaendiii Ni ajabu sana, namna moyo unahangaika (Kutafuta majibu)
Ajabu sana moyo unavyoonyesha mashaka Yakwamba japokuwa Mungu anaishi ndani yangu Kuna muda nahofu Japokuwa Mungu anaketi kati yetu Kuna muda nahofu,
Oooh nakumbuka wana wa Israel Katika bahari ya Shamu Japo walikatiza katikati ya bahari kwa ushindi
Kwa nyimbo nyingi Waliimba na kumsifu Bwana Lakini baada ya kuvuka na kuliona jagwa
Yalibadilika mambo
Manung´unikoo yalisimama Na kusahau muujiza alotenda Bwana mwanzo(Aah) Eee MUNGU Niisaidieee eee eenhee
Nikumbushe wema wako nisije laumu Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Nikumbushe wema wako nisije laumu Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Eeeh Ee MUNGU Nisaidiee
Nisaidieee Kukumbuka baba Yakwamba umenichora Kiganjani mwako
Kati ya wengi waliopo duniani eeh Na mimi umenionaa oooh ooo Nikumbushe baba Yakwamba ni wewe umeniponya nilipoumwa Yakwamba ni wewe mlipaji wa ada yangu shuleni oooh Yakwamba kama ungeniacha hatua moja Nisingelifika nilipo ooh eee Babaaa
Umenikung´uta mavumbi Kung´uta mavumbi mimi na kuniheshimisha
oooooh oooooh
Nikumbushe wema wako nisije laumu Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii
Nikumbushe wema wako nisije laumu Nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii Eeeh Ee MUNGU Nisaidiee