B Classic, 006 Na hali ya jana sio sawa na leo Mwenye mali namuona daily kwa video Ama ndio tuseme nyota yangu haijang´aa Na riziki zangu zote zimekataa
Kuomba omba ee daily kama kichaa, ndo sana Na sio kama naipenda hio hali naichukia Kamoyo kukaeka hadharani Hadi huruma, mie mnyonge kimapato Na sina lolote elimu yangu kikwazo Ninazidisha mikosi
Ama ndo basi Mi naondoka kituo, mwenzio naondoka kituo Mwenzio naumia sana Wapi hio haki? Mwenzako mimi sielewi
Hali yangu ya matambara, naonewa ee Sio kweli nakutang´ara Mwenzako hali yangu ya matambara, naonewa ee Sio kweli nakutang´ara Mwenzako hali yangu ya matambara, naonewa ee
Mbele za watu ninanuka Napopita pita kwa maduka Hata salamu wanakwepa Ati kisa mambo hayajajipa
Nimebaki mpweke sana Akili pia imevurigika Nimejikita kwenye sanaa Nione kama mambo yatajipa
Maana sielewi na tumbo linadai kila siku Na kuna wengi wameshadai huruma hakuna Majalala ndo nyumba zetu tumeshazoea Kama mabadiliko sio sana Hosana tunamuomba ee
Ama ndo basi Mi naondoka kituo, mwenzio naondoka kituo Mwenzio naumia sana Wapi hio haki? Mwenzako mimi sielewi
Hali yangu ya matambara, naonewa ee Sio kweli nakutang´ara Mwenzako hali yangu ya matambara, naonewa ee Sio kweli nakutang´ara Mwenzako hali yangu ya matambara, naonewa ee Sio kweli nakutang´ara Wapi hio haki? Mwenzako mimi sielewi