Mapenzi kizungumkuti Wenye upendo wanapigwa mabuti
Moyo wangu nyamaza Si nilikwambia ukakataa
Tazama unalia na ni leso sina eeh Sasa nifanyaje?
Aah tu usiku silali Najiuliza maswali Mwezangu anaponda raha Anabadili viwanja na baa
Aii pole pole Pole moyo wangu kwa majanga aah Pole moyo wangu kwa visanga Siwezi jisemea maumivu Pole moyo wangu kwa majanga aah Pole moyo wangu kwa visanga
Kuna muda namfungua status usiku wa manane Kisa namwangalia nikijipa moyo huenda atanipigia Lakini wapi naambulia makapi
Nimechonga mwenyewe kinanitisha Nilikotoka naye mbali amesahau Ananiliza