Wanachongachonga utadhani wamekula yasmini Maneno yao kero utadhani mwarobaini Wanachonyota wanakera utadhani nini Wao hawana shughuli, shughuli midomoni
Penzi langu napalilia Kisha namwagilia Natia mbolea ili penzi liweze kua Na likikua kisha navuna (Navuna) Najisosomoa (Najisosomoa) Mi si ndo bwana shamba Siri ya shamba ndo naijua
Aki zumbukuku, nimekubali zumbukuku
Mie zumbukuku wako my love Aki zumbukuku wananiita zumbukuku Eti zumbukuku mie wako my love
Kibarua changu manati Kuna muda narudi sipati Anakaanga chapati Imetoka iyoo
Mapenzi uchizi, bwana ukipenda Kuna muda hata uchomwe na mwiba, maumivu husikiii Na nikiwa nayeye, sitamani kula Najiona tajiri kama namiliki benki kuu
Wanachongachonga utadhani wamekula yasmini Maneno yao kero utadhani mwarobaini Wanachonyota wanakera utadhani nini Wao hawana shughuli, shughuli midomoni
Penzi langu napalilia Kisha namwagilia Natia mbolea ili penzi liweze kua Likikua kisha navuna (Navuna) Najisosomoa (Najisosomoa) Mi si ndo bwana shamba Siri ya shamba ndo naijua
Aki zumbukuku, nimekubali zumbukuku Mie zumbukuku wako my love Aki zumbukuku wananiita zumbukuku Eti zumbukuku mie wako my love