Hivi unajua Mungu ameumba dunia Na yaliyomo yote Na ametuambia tuwapende na kuwaheshimu Wanawake wote
Basi muda ulivyotimia Nami nikatafuta mpenzi wa kuishi naye Na ndo hapa nikaamini dunia ina maajabu yake Mpenzi wangu akaumwa, yakawa mekundu macho yake
Huku na huku hospitali Macho yamekoma kuona Mke wangu kawa kipofu Walimwengu wanataka nimwache
Ingawa wanakuita kipofu Mie nakupenda kwako natulianga Ingawa wanakuita kipofu Mie nakupenda kwako natulianga
Aah, natulia Nife unizike nikuzike Aah, natulia
Wanayoyasema usiogope Aah, natulia Nitakuchagua leo kesho hata na milele Aah, natulia Mwingine sina, sina kama wewe
Ukishindwa kutembea usipate taabu Nitakubeba mgongoni Hata chakula siwezi nile My love mpaka ule wewe
Na ukilala lazima nikuombee Nikukinge na magonjwa ulale salama Nami binadamu nimeumbwa Ndo maana siwezi ringa
Kesho yangu aijua muumba Matokeo Yanga na Simba
Siwezi sema eti nikuache Kisa ukipofu nitamkufuru Mungu Njoo njoo mama anaita Kama umechoka kifuani sinzia Hallo napiga guitar Wimbo mzuri kwa ajili yako
Ingawa wanakuita kipofu Mie nakupenda kwako natulianga Ingawa wanakuita kipofu Mie nakupenda kwako natulianga