Naona mnachekesha, upepo mnaupaka rangi Mnaweka siku kwenye friji na hazigandi Mnapagawa eeh, njaa baada ya shibe Mnakesha kupika mawe na mnangoja yaive
Sihitaji kuendesha gari Endesheni nyinyi maana mimi naendesha Akili za makaka mjini Usipoiva, utaula mbichi Kamata mwizi maana mie sikamatiki
Ngoja kwanza(Aaah) msinishike Dhamani ya kuku mpaka sikukuu ifike Pata potea najua hutanielewa Ni kama mwiba ulikoingia utatokea
Pumzi ndogo njiani wamekomea Leo mnavunja mwiko na jungu limekolea Kwenye hii beat ni mazishi msibane Msiba hauna gharama marehemu kafia nyumbani
Huu ni moto, wa kuotea mbali Mtoko, na sitoweza haya
Ngoma ya kitoto, pole huwezi igiza kali Jibebe, jibebe
Mwendo kasi natia gear Ukianza namalizia Ngoma lisambe spidi mia Ukiunga tela nakanyagia(Ona)
Sasa ipi mnataka? Nini mnataka? Huu mchezo mbona simple Pumzi za mrisho ngasa Tannah ni Tannah, wewe ni wewe Ingiza vifaranga ndani nakatiza mwewe
Am the winner nimepangwa na vibonde Mnatoka makamasi mnagongana ka vikombe Mtaa wa ambapo, nibebe Kinondoni Tannah, TMK ni Chege
Nitachezesha reggea nitawalewesha mbege Mtaanza kuona moshi kama disco la reggea
Watoto mwisho mtatokaga damu Mtajikuta posta mnaamkia sanamu Tannah na Bear moto hauzimi Majembe ya nini sasa? Na mjini hatulimi Jua ina giza aisee mtapotea Mi Tannah ni bahari mtajikuta mnaelea
Huu ni moto, wa kuotea mbali Mtoko, na sitoweza haya Ngoma ya kitoto, pole huwezi igiza kali Jibebe, jibebe
Mwendo kasi natia gear Ukianza namalizia Ngoma lisambe spidi mia
Ukiunga tela nakanyagia(Ona)
1,2 - 1,2 mi ndio matawi ya juu Level chafu, busu nasi Mbona mtaa yalikuuma Yaani sana tu, saana tu
Ushindi wa matuta kwenu afadhali Namba saba kwenye bukta mjihadhari Polepole bila pupa nawalaza chali Kazi chobo chenga nawapiga dali