Wanangu vipi baba mbona kimya baba Uliahidi jambo mbona kimya baba Mambo ya ndoa umefikia wapi baba Mambo ya ndoa umekwama wapi niambie
Nimezunguka dunia mzima Dunia kiganja baba, nimeyaona mengi Ya walimwengu wanasema Bora uchague mpenzi, tofauti na enzi
Wanafanana kwa sura matendo baba nko hoi eeh Unayempenda na kumwaza anamwaza meingine Bila pesa umaarufu mwonekano baba we hung´oi eeh Na kwa dunia ya sasa, nioe wapi pengine
Dunia hadaa hilo baba utambue Muda unaenda hilo uzingatie Mweke Maulana mbele mambo yatimie Dhamira yako ya kweli, nayo ajalie
Baba ooh baba ooh, daddy ooh(Baba) Najua una hamu sana, mwana Ndoa ooh, ndoa oooh, ndoa oooh
Ya mi mwanao kuiona
Kaza roho, kaza roho Dua njema atajibu Maulana Mke mwema aaah Atakuja baba
Ayee, ndoa eeh(Nuia baba) Sijamuona wa kuoa eeeh(Utaoa mwanangu) Ayee, ndoa eeh(Nuia baba) Sijamuona wa kuoa eeeh
Ng´aa tena dafaradhi Kumhalalisha mwanangu Kwangu mimi ni heshima Nikimwona mkwe wangu
Kudanga danga si kwema
Kwa leta laana mwanangu Leo Ali kesho Juma Hebu tuzao twangu
Mama wakitongoza Wanataka kuvua na nguo Ah tumejuana leo Anataka kuvua na nguo eeh
Wanaume wa sasa Suruali kushuka eeh Mama niombee kwa Mungu Nipate mwema niweze sitirika
Leta mjukuu nimwoe Aje anikojolee Ooooh, ooooh
Mama ooh mama ooh, mama ooh Najua una hamu sana Ndoa ooh, ndoa oooh, ndoa oooh Ya mi mwanao kuiona
Kaza roho, kaza roho Dua njema atajibu Maulana Mume mwema aaah Atakuja tu mama
Ayee, ndoa eeh(Nuia mwana aah) Sijamuona wa kunioa eeeh Ayee, ndoa eeh Sijamuona wa kunioa Sijamuona wa kunioa eeeh
(I say mama ma, mama...) Ayee, ndoa eeh
Sijamuona wa kunioa Sijamuona wa kunioa eeeh
Utampata baba ano kuridhia Nataka nicheze eeh, mwanangu Siku hiyo wanione eeh, mwanangu eeh Nikate, nikate, kwa furaha yangu wee eeh