đŸ’ƒđŸŽ€ Paroles de chanson Française et Internationnales đŸŽ€đŸ’ƒ

 A   B   C   D   E   F   G   H   I   J   K   L   M   N   O   P   Q   R   S   T   U   V   W   X   Y   Z   0   1   2   3   4   5   6   7   8   9 
Artiste : Bright (AF)
Titre : Soma
Elimu ni bahari isiyo na mwisho
Dada yangu soma
Njia iko huru kupambana
We kazana kusoma

Yote unayofanya leo
Future ya kesho
Amka tupa shuka
Kwenye elimu yote yawezekana

Ogopa vishawishi
Usidanganywe kirahisi
Mimba adui haichelewi
Epuka na makundi wabaya marafiki
Hakikisha haupotei

Walimu wapo wengi
Na shule zipo nyingi sana
Nyumba yaanza na msingi
Hayo mengine yatakuchanganya

Soma, we soma
Soma, we soma

Hurumie wazazi wako
Wanakusomesha kwa taabu
Wanauza vitumbua mara supu
Ili ununue kitabu

Ongoza njia tupo nyuma yako
Nyumbani usilete sababu
Una elimu mbule kwa faida yako
Serikali imetupatia

Usijeongope bila elimu hutashinda
Nenda nchi yoyote
Kama hujasoma utachakaa

Wakina Dangote
Wamebukua na chapaa
We pigana vyovyote

Elimu kwetu ni shujaa

Walimu wapo wengi
Na shule zipo nyingi sana
Nyumba yaanza na msingi
Hayo mengine yatakuchanganya

Soma, we soma
Soma, we soma

Soma, we soma
Soma, we soma