CBO baba ooh Mama haya dunia yana mambo mengi Utakuta unapenda kuishi na binadamu Lakini kila siku wanakugeukia eeh Usijali hawa ndio binadamu
Wakikukwepa kuna siku watakutafuta Wakikusengenye nyamaza watajifunza Wakikudharau ipo siku watakusifia Ni kawaida yao, kawaida yao Tenda wema nenda zako usingoje shukurani
Ona binadamu wabaya, wabaya wabaya Ubinadamu ni kazi, wabaya wabaya Watu wa dunia wabaya, wabaya wabaya Ooh no no wabaya wabaya...
Dunia sisi ni binadamu tunapita, tunapitra Dunia ya Mola, tenda mema Unajiwekea akiba kwa Mungu Baba Amini raia dunia itapita
Mungu akikujali usidharau wenzio
Ukipata kidogo saidia wasiojiweza Tenda mema duniani usingoje shukurani Kuna binadamu ni wa ajabu sana Hawapendi kuona maendeleo ya wengine
Watakuchekea usoni Ukiwapa kisogo wanakumaliza kabisa Hawana maana Watakufuata kama unacho Ukikosa kabisa wanakumaliza kabisa Ni binadamu
Mwenzako akipata usinune Fanya na wewe ujitume Chuki hawezi kuwa mfalme Ndo maana lima kesho uvune
Mwenzako akipata usinune
Fanya na wewe ujitume Chuki hawezi kuwa mfalme Ndo maana lima kesho uvune