Bwana Yesu ninakushukuru Nina kila sababu ya kusema asante Kwanza kwa zawadi ya uzima Lakini pia kwa yale yote mema uliyonitendea
Hata kwa yale ambayo sijaona kwa macho ya nyama Wacha niseme asante Maana najua kwa wakati wako utayatenda
Baba asante kwa milima Baba asante kwa mabonde Asante kunipigania vita Umenifanya dhahabu safi Baada ya moto mkavu
Asante kwa hatua nyingine Na ngazi nyingine Natamani siku moja niitwe Mbarikiwa wa bwana Maana neno lako linasema Unatuwazia mawazo mema Tena ya amani ya kutupa tumaini Siku zetu za mwisho