Unikumbuke Baba Unapowazuru wengine naomba unikumbuke Usinipite Yesu Unapowazuru wengine naomba unikumbuke
Unikumbuke Baba Unapowazuru wengine naomba unikumbuke Usinipite Yesu Unapowazuru wengine naomba unikumbuke
Unikumbuke, unikumbuke Unikumbuke, unikumbuke Yesu naomba unikumbuke Usinipite, usinipite Usinipite, usinipite Yesu naomba unikumbuke
Mnyonge mimi dhaifu mimi, unikumbuke Na mama utaka kunyonyesha, umkumbuke Ona huyo asiye na kazi, mkumbuke Lazima na wajane wanalia, uwakumbuke
Kijana huyo ataka mwenzi, umkumbuke
Na mwingine huyu ataka elimu, umkumbuke Umasikini sasa ndio wimbo, utukumbuke Nchi nzima vilio vimetanda, utukumbuke
RUnikumbuke, unikumbuke Unikumbuke, unikumbuke Yesu naomba unikumbuke Usinipite, usinipite Usinipite, usinipite Yesu naomba unikumbuke
Ewe mwenyezi Mungu mwenye rehema; mwingi wa utukufu Bwana wa viumbe vyote Muumba wa mbingu na dunia Twakuomba kwa unyenyekevu utupe hekima na busara
Sisi waja wako tuliokusanyika hapa
Uibariki Tanzania iwe nchi ya amani Na wote wanaoishi humo wawe na upendo halisi na umoja
Serikali yetu na viongozi, uwakumbuke Waongoze nchi kwa hekima yako, uwakumbuke Uchumi wa nchi yetu Baba, uukumbuke Bunge pia na mahakama, uikumbuke
Sikia kilio cha watanzania, utukumbuke Majibu ya matatizo yakoke kwako, utukumbuke Tazama majanga yanayotukumba, utukumbuke Ajali nyingi twazika wengi, utukumbuke
Unikumbuke, unikumbuke Unikumbuke, unikumbuke Yesu naomba unikumbuke Usinipite, usinipite
Usinipite, usinipite Yesu naomba unikumbuke