đŸ’ƒđŸŽ€ Paroles de chanson Française et Internationnales đŸŽ€đŸ’ƒ

 A   B   C   D   E   F   G   H   I   J   K   L   M   N   O   P   Q   R   S   T   U   V   W   X   Y   Z   0   1   2   3   4   5   6   7   8   9 
Artiste : Harmonize
Titre : Amen
Amen, Amen
Amen, Amen
Amen, Amen
Nenda salama kipenzi

Amen, Amen (Iyee eh eh)
Amen, Amen (Iyee eh eh)
Amen, Amen
Tutazidi kukuenzi

Tunakushukuru kwa yote
Mazuri ulotufanyia
Hii safari ni yetu sote
Leo mwenzetu unatangulia

Nenda, nenda salama
Tutaonana kesho kiama
Poleni ndugu na jamaa
Pumzika unaiacha alama

Mungu Baba wa mbinguni
Anayetoa ndo ametwaa
Umetuacha na huzuni

Tumeshikwa na butwaa

Kukupoteza kipenzi cha wengi
Ulopambana kwa ajili ya wengi
Mungu akulaze mahala pema
Umeondoka bado mapema

Kama sio juhudi zako Mkapa
Jengo jipya la bunge Dodoma
Tungelipata wapi?

Oooh kama sio juhudi zako Mkapa
Na uwanja wa taifa
Tungeupata wapi?

Kama sio juhudi zako wewe Baba
Na daraja la Mkapa
Tungelipata wapi?

Oooh Amen! (Amen, Amen)
Oooh Amen! (Amen, Amen)
Amen (Amen, Amen)
Nenda salama kipenzi

Amen, Amen (Baba nenda)
Amen, Amen (Tunakupenda)
Amen, Amen (Nenda baba nenda)
Tutazidi kukuenzi

Ama kweli vizuri havidumu
Kazi ya Mola hauwezi kuilaumu
Ulipambana na udhulumu
Vita zidi ya rushwa

Kipenzi chetu umetangulia
Umetuachia majonzi

Taifa nzima tunalia
Kukurudisha ndo hatuwezi

Kama sio juhudi zako Mkapa
Uchumi imara
Tungeupata wapi?

Oooh kama sio juhudi zako Mkapa
Ukweli na uwazi
Tungeupata wapi?

Oooh Amen! (Amen, Amen)
Amen! (Amen, Amen)
Amen! (Amen, Amen)
Nenda salama kipenzi

Amen, Amen (Basi nenda)
Amen, Amen (Japo tunakupenda)

Amen, Amen (Nenda baba nenda)
Tutazidi kukuenzi