Sitaki nipeni mji (Weh nenda Dar Es Salaama) Masela nataka mji (Nenda Dar Es Salaama)
Mh, hilo jiji bwana kuishi ujipange Dada ukitaka gari ni lazima udange Hadi wamaasai wana namba za Mange Ama niende Mbeya? Tulia atanipokea, ila Dar siwezi sogea Kazi kubeti na umbea Arusha, naona kama nitajirusha (Bomboclaaa-) Keramutu ni Moshi, vipi mimoshi
Naiwaza sana Dodoma Ila moyo bado una goma Mh, au niende Kigoma Ama nipelekeni alipo Roma (Alright)
Ngoja kwanza, wacha niende Mwanza Nikale sato kwanza ila mh, Mtwara kwanza Eti huko Bongo Vitu vidogo, vidogo wanaume wanasusa Kila mwenye kiki kidogo anatembea na baunsa (Shit)
Nataka mji (Nenda Dar Es Salaama) Sitaki nipeni mji (Weh nenda Dar Es Salaama) Masela nataka mji (Nenda Dar Es Salaama) Wanazunguka kwa waganga wakikosa Wanarudi kwa Mwamposa Tajiri hanaga makosa Machinga nafasi kakosa Joto la Dar, lazima uwe na AC Muda mwingine umeme unakata kumshinda Ray C
Kama nitasogea, sogea ni Morogoro au Songea
Wanaume wa Dar kwa kuongea, na pa kulala wanagongea Mm, mh Yasikutishe maisha yao ya kwenye TV Buti, jeans na t-shirt, fake Louie V Wabongo hawakupi mishe hata kama uwe na CV Ukiacha Iringa na Njombe, Dar pia kuna HIV Vitu vidogo, vidogo wanaume wanasusa Kila mwenye kiki kidogo anatembea na baunsa (Shit) Nataka mji (Nenda Dar Es Salaama) Sitaki nipeni mji (Weh nenda Dar Es Salaama) Masela nataka mji (Nenda Dar Es Salaama)