Asubuhi imefika, anga inang´aa mvua imaanza katika, ghafla tumbo la njaa naweka sauti kwa spika, nipate umbea wa dar mara simu inaita jina la anko twaha akisema, mama yu hoi kitandani kama si wa leo wa keaho na kupona sizani upate japo neno la mwisho mi ndo mtoto wa pekee nyumbani wananitegemea mdogo wangu wa kike tayari dunia alishaondolewa tizama jasho langu la mnyonge kipato hakikidhi mahitaji
napiga moyo konde yarabi mola ndo mpaji
Matatizo. matatizo yatakeisha lin matatizo kila siku mimi ewe mola. matatizo yatakwisha lini japo likizo nifurahi na mimi.
Mola aliniumba na subira imani pekee ngao yangu Mbona nishasali sana ila mambo bado tafalan mama kanifunza kikabila nikonde sana haini yangu
tena nijitume sana na vya watu nisivitamani hta mpenzi niliyenae najua siku atanikimbia itanitesa ye ndo nguzo zile ngoja kesho badae atazichoka kuzivumilia anakosa hata matunzo ona, nadaiwa kodi nilipopanga nashinda road nikihanda nishapiga hodi kwa waganga kwa kuhisi narogwa nokauza maji na karanga nikawa dobi kwa viwanda ila kote ziro ni majanga mtindo mmoja
mi ndo mtoto wa pekee
nyumbani wananitegemea mdogo wangu wa kike tayari dunia alishaondolewa tizama jasho langu la mnyonge kipato hakikidhi mahitaji napiga moyo konde yarabi mola ndo mpaji