Natamani niandike barua, na niitume kwako Ilanahisi hutaisomaa, utaikataa
Hata simu nitajisumbua, kupiga namba yako Maana hata ukiiona utaikata
I wish yawe ndoto, haya ninayo yapitia Ama nirudi utoto imenisonga dunia Eti kurwa bila ndoto, hivi ni wapi ntaanzia? Kulia bila kushoto, sijawai kusikia
Eeh, imagine siwezi kukuota (aah aah aah) Maana ata usingizi sina (Sinaa) Mwenzako wataniokota (aah aah aah) Maji yamenizidi kina (Mwenzenu mimi) Mpaka kesho, eeh eeh Mpaka kesho, umeniganda mawazoni Mpaka kesho, bado nakuwazaa Mmh mmh eeh Yaani mawazo kizunguzungu (Mpaka kesho) Insta napaona pachungu (Mpaka kesho)
Mateso nihurumie (bado nakuwaza)
Nishajaribu kudanga nipoteze mawazo, huenda nitaenjoy Kumbe najivua utu na heshima Kwa watabibu waganga Nijue nini chanzo, mwenzako nipo hoi Ama nyota yangu butu, makali sina
Eeeh, zile nadhiri Kwamba utaniweka moyoni zinajirudia Mie ndio moja we mbili Mbona sasa sikuoni, umenikimbia Mie mwenzako ka sabuni kichelema Siezi ata kupangusa ah ah Jeraha la penzi nachechema Sina furaha ata ya kunusa ah ah Yaani umeniacha dillema
Siwezi kupanda kushusha ah ah Yaani mapenzi vitaa, CCM na Chademaa Firauni na Musa ah ah
Eeh, imagine siwezi kukuota (Aaah aah aah) Maana ata usingizi sina (Sinaa) Mwenzako wataniokota (Aaah aah aah) Maji yamenizidi kina (Mwenzenu mimi) Mpaka kesho, eeh eeh Mpaka kesho, umeniganda mawazoni Mpaka kesho, bado nakuwazaa Mmh mmh eeh Yaani mawazo kizunguzungu (Mpaka kesho) Insta napaona pachungu (Mpaka kesho) Mateso nihurumie, (bado nakuwaza)
Wa kumove on nitakuwa mie (oh siwezi) Yaani ipite siku nisikufikirie (oh siwezi)