Ni mwaka mpya mambo mapya sina dhambi nimetubu Na pesa ntazichanga change nizijaze kwa kibubuu Japo hata kakibanda nikajenge huko pugu Maana nyumba za kupanga nishazichoka vurugu Eti kwani wao waweze wana nini (Mmmh) Na mimi nishindwe nina nini Nishachoka siku zote kuwa wa chini Wengine wanakula kipupwe ma ofisini
Mwaka huu ni wangu kutimiza ndoto zangu Nasema mwaka huu ni wangu kwa baraka za mungu wangu, dear Lord Hakuna mungu kama wewe babaa (Eh, hakuna) Kama wewe yawee (Eh, hakuna)
Hakuna mungu kama wewe babaa (Eh, hakuna) Kama wewe yawee (Eh, hakuna)
Huu mwaka nakusanya mavumba ninunue gari yangu Na wale waliosema mimi ni mguma waje wamuone mwanangu Huu mwaka marafiki wasio na faida nawaweka pembeni Wanaokufata wakati wa shida ili wapate hafueni Niwaonyeshe walionidharau kama mungu anaweza Nami nipande dau niwasalimu kingereza
When God say yes nobody can say no (When God say yes nobody can say no) When God say yes nobody can say no (When God say yes nobody can say no)
Mliosema haolewi olewi mbona kaolewa
Mliosema hapewi hapewi mbona amepewa
Mwaka huu ni wangu kutimiza ndoto zangu Nasema mwaka huu ni wangu kwa baraka za mungu wangu, dear Lord Hakuna mungu kama wewe babaa (Eh, hakuna) Kama wewe yawee (Eh, hakuna) Hakuna mungu kama wewe babaa (Eh, hakuna) Kama wewe yawee (Eh, hakuna)