Mi na yeye tuungane kuwateketeza maadui Eeh maadui Badala ya miezi kupita aah Vikombe lazima vigongane Na sio kwamba hayajui, eeh hayajui
Pigo za kusema vya ndani mi sinaga hizo Ama kumtafuta mchawi ni nani ni kuongeza tatizo Tulia hapa tutakuwa wa ndani hadi paradiso Na tukatangaza kweupe mambo ya hadharani Na tattoo ndo hizo, oh oh ohhh
Sitaki kuamini kwamba Lile kapu la mabaya yangu Halina hata machache mema oh mema Nitakuwa mshamba Nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu Ili nionekane mwema
Japo mapenzi yanaumiza I wish tusisemane (Vibaya vibaya) Ili kesho tusizikane (Vibaya vibaya) Usiwasikilize wapambe (Vibaya vibaya) Wanachotaka maneno ili kesho watuchambe (Vibaya vibaya)
Oa aaah, oooh aaah Oooh aah...ooooh mmmh
Nitunzie siri zangu Nami nitunze zako za miaka rudi nenda Kuna leo na kesho mmh mmh mmh Hata maadui zangu walikuwaga maadui zako Hawawezi kukupenda wanakuvuta uwe kichekesho
Mmmh mmh mmh
Maana hata ukisambaza Picha zangu za aibu ni sawa, hata hunikomoi Na hata utupu wako ukiutandaza Kwa watu wangu wa karibu sio doa, hujengi hubomoi
Mama kuna kamchezo mtunze mtoto wako Na watu wenye majungu (Majungu) Nilikubali kuviacha vya dezo Sababu ya mapenzi yako nikaachana na mzungu (Mzungu)
Maneno yao utadhani wanakutetea Kumbe tudhalilishane wanachongojea Usiwape faida wambea Na ni kama kawaida nakuombea
Sitaki kuamini kwamba Lile kapu la mabaya yangu
Halina hata machache mema oh mema Nitakuwa mshamba Nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu Ili nionekane mwema
Japo mapenzi yanaumiza I wish tusisemane (Vibaya vibaya) Ili kesho tusizikane (Vibaya vibaya) Usiwasikilize wapambe (Vibaya vibaya) Wanachotaka maneno ili kesho watuchambe (Vibaya vibaya)
Oa aaah, oooh aaah Oooh aah, ooh aah...ooooh mmmh
(Konde Music Worldwide) B Boy thank you for the sound Sound...Sound