Tangu nikuwe tumboni mwa mama Mungu aliniona Na licha ya mavumbu na mapito Vikwazo kila kona
Wakipanga mabaya anapangua Wema na wabaya anawajua Mitego wanatega anategua Na hali si zetu anatambua
Yalinitesa mawazo Mbele giza sikuiona njia Vikawa vingi vikwazo Niliumia sana
Yalinitesa mawazo Mbele giza sikuiona njia Vikawa vingi vikwazo Niliumia sana
Machozi yamekauka, sitolia tena Sitalia, sitolia tena Sitolia tena, sitolia tena
Nishajua Mungu yuko na mimi
Machozi yamekauka, sitolia tena Sitalia, sitolia tena Sitolia tena, sitolia tena Nishajua Mungu yuko na mimi
Najua atapangua, ooh bwana atapangua Ooh najua atapangua, Mungu wangu atapangua Mitego yote atapangua, ee Bwana atapangua Watesi wote ataondoa, ee Bwana atapangua eeh