I sing for you mama I love you ma(Mama mama) I love, I love you ma(Mama mama)
Maneno yako na busara zako
Zinazunguka kichwani mwangu Popote nilipo upo mama Unasema na moyo wangu
Kwenye mazito na magumu Usia wako ndo ngome yangu Hupendi nikijilaumu Nikipatacho ndo fungu langu
Ulisema mama, narudi utoto(Ooh) Moyo unaniwaka moto Jinsi ulivyoniendo usiku haulali(Ooh) Vihoma homa ama baridi kali Ukanilinda kama mboni yangu
Hata kama nikisema nikushukuru Pesa na mavogi bado Hata nijenge nyumba mithili ya ikulu
Kufikia upendo wako bado
Hata kama nikisema labda nikushukuru Pesa na mavogi bado Hata nijenge nyumba mithili ya ikulu Kufikia upendo wako bado
Kwa taani udhalilike(Huruma yako mama) Ukanyage miba mi nipite(Huruma yako mama) Ushinde na njaa mi nishibe (Huruma yako mama) Ukanyage miba mi nipite(Huruma yako mama)
I sing for you mama I sing for you mama
Mama, hii ni yako mama Ulichana nguo zako nistiri mwana Mama, wa kupendwa sana
Walivumilia leba walipotupata
Wapo walokataliwa(Mama) Na milango kufungiwa(Mama) Nyumbani kutimuliwa(Mama) Na mali kudhulumiwa(Mama) I love you ma
Hata kama nikisema labda nikushukuru Pesa na mavogi bado Hata nijenge nyumba mithili ya ikulu Kufikia upendo wako bado
Hata kama nikisema labda nikushukuru Pesa na mavogi bado Hata nijenge nyumba mithili ya ikulu Kufikia upendo wako bado
Kwa taani udhalilike(Huruma yako mama) Ukanyage miba mi nipite(Huruma yako mama) Ushinde na njaa mi nishibe (Huruma yako mama) Ukanyage miba mi nipite(Huruma yako mama)
I love you ma I love, I love you ma I love you ma I love, I love you ma