Hapo ndipo mfalme wa haki atakapotawala Hapo ndipo mfalme wa kweli atakapotawala Maana dunia ya leo watu wanapendeleana Maana dunia ya leo watu wanapendeleana
Atatawala mwenye dunia Atatawala mwenye watu wake Maana dunia ya leo watu wanapendeleana Maana dunia ya leo watu wanapendeleana
Hapo ndipo falme zote za dunia zitanyamaza Mwenye wa kweli atawala Atasimamia mahakama zote kwa haki Atasimamia kesi zote kwa haki Kila mmoja atalipwa sawa
Dunia yote itatiishwa kwenye uweza wake Dunia yote itashangaa alivyo wa haki
Mataifa watajua yeye ni mwema
Hapo ndipo wote tutajua kwamba yeye ni Baba Dunia yote itaelewa ni mhukumu wa haki Maana dunia ya leo watu wanasaidiana Maana dunia ya leo watu wanasaidiana
Atatawala asiyejua pendelea mwingine Watu wa leo wanatazama sifa ya mtu
Majira yanakuja ya kujua Baba wa kweli Majira yanafika watamjua Mungu wetu Leo hawatambua machozi tunayolia Leo hata ukilia hakuna wa kutazama
Hata ukiteswa hakuna wa kutazama Wakati unakuja Baba atatawala kwa haki Hapo ndipo falme zitajua yeye ni mfalme
Hapo ndipo dunia itaelewa yeye ni Bwana
Tutapanguzwa machozi yetu na sisi Tutapanguzwa machozi yetu na sisi Tutaheshimiwa na dunia na sisi Tutaheshimiwa na watu wote na sisi
Hawawezi tambua haki yako leo hii Maana dunia ya leo watu wanasaidiana Hakuna wa kutetea maisha yako Maaana tawala za leo wanapendeleana
Anakuja mtawala wa haki kutusaidia Anakuja mtawala wa haki kutusaidia
Utafurahi na Baba Tutashangilia kwa Baba Maana falme wake Baba itakuwa ni yenye haki