Wa kupewa sifa ni wewe Bwana Na utukufu wote ni wewe Bwana Wa kupewa sifa ni wewe Bwana Na utukufu wote ni wewe Bwana
Maana wewe wazistahili zote Maana wewe peke yako ni Mungu Maana wewe wazistahili zote Maana wewe peke yako ni Mungu
Utukuzwe
Juu mbinguni hakuna wa kufa´na nawe Humu duniani hakuna mfano wako Chini ya nchi hakuna kabisa U juu ya yote, u wa pekee Una mamlaka yote Bwana Hakuna Mungu kando yako Yahweh
Unayetuokoa a Bwana Unayetutegemeza twakusifu Watutia nguvu za kuendelea Tunapochoka watuhimarisha
Kwa rehema na neema zako Mwokozi Hakuna kama Wewe Hakuna kama We Hakuna kama wewe e Yahweh eee
(U wa neema Yesu na mwingi wa rehema)
U wa neema Yesu na mwingi wa rehema Kwa neema yako Messiah umetuleta hapa Katufilia msalabani tupate wokovu Tunayashinda majaribu kwa neema yako
Wengine tulisahaulika ´katumbuka Baba Toka mavumbini ´katuketisha na wafalme Umetufanya ufalme na makuhani wako Tunakuinua leo Yesu u wa neema