Adui zangu, nimewasamehe bure Na moyoni mwangu sina kinyongo tena Watesi wangu nimewasamehe bure Na moyoni mwangu, nimejaza msamaha
Moyo wangu una amani Moyo wangu hauna mashaka Moyo wangu una furaha Moyo wangu hauna kinyongo
Moyo wangu una amani Moyo wangu hauna mashaka Moyo wangu una furaha Moyo wangu hauna kinyongo
Matukio ni mengi katika dunia Na wanaotuudhi ni wengi mno Na wengine ni wale wa karibu nasi Tutaweka wangapi katika mioyo
Matukio ni mengi katika dunia Na wanaotuudhi ni wengi mno Na wengine ni wale wa karibu nasi
Tutaweka wangapi katika mioyo
Mwisho mioyo yetu ipasuke bure Mwisho sura zetu, zizeeke mapema
Mwisho mioyo yetu ipasuke bure Mwisho sura zetu, zizeeke mapema Rahaaaa jipe mwenyewe...
Moyo wangu una amani Moyo wangu hauna mashaka Moyo wangu una furaha Moyo wangu hauna kinyongo
Moyo wangu una amani Moyo wangu hauna mashaka Moyo wangu una furaha Moyo wangu hauna kinyongo
Ugomvi ni mbaya, huumiza moyo Kinyongo ni hatari, hukosesha raha Kwa nini ujitese kwa mambo yapitayo Hao ni wanadamu, wanapita tu
Ugomvi ni mbaya, huumiza moyo Kinyongo ni hatari, hukosesha raha Kwa nini ujitese kwa mambo yapitayo Hao ni wanadamu, wanapita tu
Hata wasipotubu, wewe wasamehe Usijinyime raha jipe mwenyewe
Hata wasipotubu, wewe wasamehe Usijinyime raha, jipe mwenyewe Nasema raha jipe mwenyewe...
Moyo wangu una amani Moyo wangu hauna mashaka Moyo wangu una furaha Moyo wangu hauna kinyongo
Moyo wangu una amani Moyo wangu hauna mashaka Moyo wangu una furaha Moyo wangu hauna kinyongo
Adui zako, wewe wasamehe bure Na moyoni mwako usiwe na kinyongo Watesi wako we wasamehe bure Na moyoni mwako ujaze msamaha
Binadamu wengine ni wakorofi Hata ukinyamaza, watasema tu Ajira yao kubwa ni masengenyo
Usigombane nao, utakosa nguvu
Binadamu wengine ni wakorofi Hata ukinyamaza, watasema tu Ajira yao kubwa ni masengenyo Usigombane nao, utakosa nguvu
Ukifanikiwa wanakasirika Kama waliyachangia, mafanikio yako Mungu akikuinua mioyo inawauma Kama walijuwa agano lako na Mungu Ukifanikiwa wanakasirika Kama waliyachangia, mafanikio yako Mungu akikuinua mioyo inawauma inawakera Kama walijuwa agano lako na Mungu Mie Raha Najipa Mwenyewe...