Katika maisha yangu Nilipokea wageni Nikawakaribisha kwangu Wakafanya vitu vingi Hawakuwa wa kudumu
Walikuwa wapitaji Ila moyo wa ukarimu Ukanisababishia machozi
Mgeni wa kwanza alikuwa ni uchungu Akaniumiza, akanipa maumivu Alipomaliza akaenda zake Mgeni wa pili alikuwa ni huzuni Huyu naye Akanikosesha furaha Mgeni wa tatu alikuwa ni magonjwa Akanidhoofisha, akataka kuniua Hakufanikiwa akaenda zake
Aliyefuata alininyima watoto Jina lake tasa Naye alipita
Mgeni mmoja jina lake ni mauti Akamchukua Ntimi, akaniachia jeraha
Mgeni mwingine jina lake hofu Hakutaka nifanikiwe Akanipa fikra potofu Nikajiona siwezi Tena nitafeli Huyo naye alipita
Hawa ni wageni Tena wapitaji Hawatadumu, watapita Hawa ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita
Hakuna jambo lolote gumu Litakalodumu kwenye maisha yako
Ila yote yatapita Na yakishapita Hayatarudi tena
Tough times never last But tough people do
Mapito siyo mambo magumu unayoyapitia kwenye maisha yako Ila mapito ni mambo magumu yanayopita kwenye maisha yako Ndiyo maana ninaita mapito, kwa kuwa yanapita tu Na yanapita kwenye maisha yako, Na yakishapita hayawezi kurudi tena, ah
Magonjwa, Hao ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita
Uchungu, (Huzuni) Hao ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita Mateso, (Changamoto) Hao ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita (Hata dhiki) Hao ni wageni, tena wapitaji Hawatadumu, watapita