[Diamond Platnumz:] Oooh hizo ni zama za kale Oooh Sangulo na pepe kale Zilipendwa
[Rayvanny:] Eh! Kizamani,kutoa card na maua (zilipendwa) Wanataka money ukilipa unakwarua (zilipendwa) Ufundi kitandani,sio maguvu kujikwamua (zilipendwa) Unafika ndani,hujatomasa unachanua (zilipendwa) Wanawake wa leo wanataka mikakati Ukiwa mzugaji haki ya mungu huwapati (zilipendwa) Mapenzi ya video yatakutoa kamasi Eti nikinywa maji nakuona kwenye glass (zilipendwa) Eeh! kupiga chabo getto (zilipendwa) Mkono na dettol (zilipendwa) Sunche na kapeto (zilipendwa) Majay na Mobeto (zilipendwa)
[Diamond Platnumz:] Oooh! Hizo ni zama za kale
Oooh! Sangulo na Pepe kale Mmm boringo ndombolo (zilipendwa) Twanga chipolopolo (zilipendwa) Na maji ya kandoro (zilipendwa) Simba wa Morogoro (zilipendwa)
[Rich Mavoko:] Mtaani sipati sukari guru kabisa (zilipendwa) Hivi yuko wapi Mb Dogg wa Latiffa (zilipendwa) Babu Tale wapi papa misifa (zilipendwa) Siku hizi party hatuendagi Ibiza (zilipendwa) Mpira na Pele (zilipendwa) Tanu na Nyerere (zilipendwa) Asha Ngedere (zilipendwa) Harusi mabele (zilipendwa) Eeeti Uuze nyumba uweke heshima bar Eeeti Ulazimishe aliyekukataa Sabuni Kicherema (zilipendwa)
Mabanda ya Cinema (zilipendwa) Lipumba na Mrema (zilipendwa) Diamond na Wema (zilipendwa)
[Diamond Platnumz:] Ooooh hizo ni zama za kale (zama za zamani) Ooooh Sangulo na pepe kale (yoyoyo) Mmm Aggy na sogi dogg (zilipendwa) Chanel analog (zilipendwa) Movie za saibog (zilipendwa) Van Damme Arnold (zilipendwa)
[Queen Darleen:] Una nibeep nikupigie umeiweka vocha (haloo) Ule wewe nilipe mie umeniona Loffa Teena na madada wenye majina acheni visa Unaitwa ukale dinner mnakwenda Tisa Nywele za kichina (zilipendwa)
Pochi za kuazima (zilipendwa) Zena na betina (zilipendwa) Bashite gwajima (zilipendwa)
[Diamond Platnumz:] Ooh hizo ni zama za kale (zama za zamani) Ooh Sangulo na pepe kale (yoyoyo) Mmm Amitabh Bachchan (zilipendwa) Tv kwa jirani (zilipendwa) Madee Rayvany (zilipendwa) Zai Ivan (zilipendwa)
[Harmonize:] Yanini kunichunguza naishi wapi (zilipendwa) Nala,chapati kwa maini au makapi (zilipendwa) Kutwa kunikalia chini unda kamati Oh ya Rabi masikini kuni dhihaki Ah Samba Mapangala (zilipendwa)
P Funk Kajala (zilipendwa) Onyango na Jangala (zilipendwa) Rufufu mkandala (zilipendwa) Vya nini vidomo domo tutupiane tunguli Kisa pesa za mkopo msimu wa Magufuli Ah, Bongoman yondo (zilipendwa) Sikinde Msondo (zilipendwa) Magari ya Udongo (zilipendwa) Babu wa Loliondo (zilipendwa)
[Diamond Platnumz:] Ooooh hizo ni zama za kale (zilivumaga sana) Ooooh Sangulo na pepe kale (yoyoyo) Ah Tv za kichogo (zilipendwa) Wakina Man Dojo (zilipendwa) Aggy na Iyobo (zilipendwa) Akina Hatupogo (zilipendwa)
[Mbosso:] Eti msiba ukiona Bundi unataka kupagawa Tulale makundi makundi kuogopa popo bawa Zuwena nitampata wapi (zilipendwa) Zuwena wa zile nyakati eh (zilipendwa) Kujifanya mapanga sunna eti wamepinda Wengine wabeba vyuma na hakuna marinda Iddi Amini dada (zilipendwa) Miuno ya H Baba (zilipendwa) Domo Chai Jabba (zilipendwa) Michezo ya kibaba baba (zilipendwa)
[Lava Lava:] Wale wapiga madeal sasa hali mbaya (zilipendwa) Hizi zama za Magufuli si za Jakaya (zilipendwa) Ugomvi wa Mr.Nice na Dudu Baya (zilipendwa) Vikatuni vya madenge baba ubaya (zilipendwa) Muhogo mchungu Mr. Bean, wapi bambo (zilipendwa)
Wale wazamiaji wale wa melini wazee wa ng´ambo Hivi yuko wapi Banjamini wa Mambo Jambo Wa Vietnam waporini vita na Rambo Eh ndanda Mjela jela (zilipendwa) Kidali Kombolela (zilipendwa) Max na Zembwela (zilipendwa) Juma Nature na fela (zilipendwa)
[Diamond Platnumz:] Ooooh hizo ni zama za kale (zama za zamani) Ooooh Sangulo na pepe kale (yoyoyo) Mmm kamanda Daz Nunda (zilipendwa) Kalumanzila Ndumba (zilipendwa) Simu za Dole gumba (zilipendwa) Johari na Kanumba (zilipendwa)