Dunia imejaa visanga Ubinadamu umekuwa majanga Tembo amefungwa kwa banda Anataka kula kuku pia na vifaranga
Mungu tu akusamehe Wewe ni kama ndugu yangu Upunguze ma ugali Uadui wa nini mwenzangu we
Ukitenda kosa na haujaomba radhi unakosea (Kosea) Mama yake mzazi huruma ungemwonea (Mwonea)
Chunga kinywa kiwe na kituo Hekima ndo iwe funguo Maneno ya nini? Unajivua nguo Kumbuka ulimwengu ni kama chuo
Ungenyamaza, bora ungenyamaza Kaa kimya kama huna la maaana Ungenyamaza, bora ungenyamaza Ukikosa heshima bora kukaa kimya Ungenyamaza, bora ungenyamaza Bora ungenyamaza Ungenyamaza tu, bora ungenyamaza Kuwa muungwana
Mmmmh hasira hasara Mimi ni ndugu yako kanitoa kafara Ukakesha hukutaka kulala Ukipambana niharibikiwe kaka wa Mtwara
Ukasahau mapenzi ni siri Tena siri ya wawili Kilichokuponza maadili Tamaa ukashindwa isitiri
Tunza heshima yako Na mashabiki wako hadi mbungeni Na unapotongoza warembo Boxer usiweke pembeni