Kama umekaa upande wa maadui basi jipange Na kama umekula kuku na bia za wafilisti Utazitapika, maana hii Lazima ing´oke na mtu
Walimnyoa nywele za usoni wakasema wameshamweza Wakamtuma gerezani wakadhani wameshammaliza Walisahau siri ya Samson ni nywele zake Walisahau kwamba nguvu za Samson ni nywele zake
Zimeota tena, zimeota tena Nywele zimeota tena, zimeota tena Kamba zimekatika, zimekatika Minyororo kukatika, imekatika
Kamba zimekatika, zimekatika Minyororo kukatika, imekatika Kumbe zimeota tena, zimeota tena Nywele zimeota tena, zimeota tena
Walikaa na kwa waganga ili waweze kufuta jina lako Wakatoa na kafara ili wakatishe uhai wako Waliteta na kuzimu ili waharibu mambo yako Walisahau kwamba mkono wa Mungu pamoja nawe Walisahau kama neno la Mungu li pamoja nawe
Kumbe zimeota tena, zimeota tena Nywele zimeota tena, zimeota tena Kumbe zimeota tena, zimeota tena Nywele zimeota tena, zimeota tena