Ukipata mia mbili shukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa
Wewe tulia mshukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa
Yatakutoa roho Wacha kwenda mbio mbio Usishindane na huyo Wewe nenda pole pole, pole pole Maisha ni pole pole, pole pole
Mungu ameumba dunia riziki mafungu saba Wewe imba mapambio Pengine la kwanza na la pili si lako La kwako saba we, tulia imba mapambio
Wacha kutamani vitu vya wengine Vinaumiza moyo
Wewe imba mapambio Ridhika na ulicho nacho
Wewe tulia mshukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa
Ya watu yatakutoa nyongo Unataka mapesa kama ya fulani utatoa wapi? Wewe imba mapambio Wataka utajiri kama wa fulani hujui alipataje? Wewe imba mapambio
Fulani ana utajiri na hujui agano lako Kama itakutoa nyongo Mumeo kipato chake ni buku Hafanani na fulani, mwombee imba mapambio
Wewe imba mapambio, shukuru Mungu Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa
Ukipata mia mbili shukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa Yatakutoa roho
Wataka mrembo wa gharama kama Wema Sepetu Kwa kipato cha Harmo Rapa we yatakutoa nyongo Chunga atakutoa roho
Mrembo ana level ya pizza Kipato chako miguu ya kuku, chunga atakutoa roho Wewe imba mapambio, shukuru Mungu Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa
Dunia ina mambo, ina mambo Vituko na vijambo na vijambo Siri nyumba ya mgongo, ya mgongo Usishindane na huyo