Nimechoka mateso Nimechoka tabu Baba mungu naja kwako Nibariki na mimi Kila siku taabu
Kila siku kilio Machozi na huzuni baaba Wenzangu wananicheka Nipitapo kwenye taabu Baba naja kwako Nibariki na mimi Nimechoka kutamani vitu vizuri vya wenzangu Nami nakuja kwako Nibariki na mimi Ikiwa ni laana Ikiwa ni mikosi Ilikwisha msalabani baaba Neno lako linasema Niite nitaitika Nami nakuita bwana Nibariki na mimi Nibariki nibariki nibariki Bwana
Nibariki nibariki uniguse bwana
Majirani wananishanga Wengine wananichekaa Eti! kwasababu ya shida mimi Nimekua kituko nikipita kwa wenzangu Nimekua kichekesho mimi Watoto wangu wana shida Ndugu zangu wantaabu Yesu nakuja kwako Nikumbuke bwana Nami nimekua mumini Nami nakungojea uje Kwako nanyenyekea Nibariki na mimi Nimechoka mateso baba Nimechoka kilioo Nimechoka taabu