Mwambieni yule mbweha, nimerudi kutoka njangwani Nimesimama tena kwenye zamu yangu Wapeni habari wale umbwa Hii si bahati mbaya, mbingu zimeniamini Mungu amenidhibitisha
Mpe salamu Yezebeli Nimerudi kutoka njangwani Nimesimama tena kwenye zamu yangu Wapeni habari wale umbwa Hii si bahati mbaya, mbingu zimeniamini Mungu amenidhibitisha
Mimi simba wa kike Kuwinda ndio asili yangu Nitawinda popote, nitaguruma popote Mbele ya mnyama wowote, kwenye pori lolote Katika nyakati zote, sitaogopa chochote Sitanyamaza hadi Mungu atakaponitwalia utukufu
Jeuri yangu, kumcha bwana ndio jeuri yangu Kumcha bwana ndio fahari yangu Kumjua Mungu ndio jeuri yangu Kumcha bwana ndio jeuri yangu
Simba lelele (Mawindoni niko mawindoni) Simba anaguruma leo (Mawindoni niko mawindoni) Simba wa kike anaoguruma leo, simba wowowo (Mawindoni niko mawindoni)
Kumcha bwana ndio jeuri yangu, simba Kumjua Mungu ndio jeuri yangu, simba yeyee Malengo yangu mimi ni Mungu wangu, simba yeyee Fahari yangu mimi ni Mungu wangu, simba yeyee Simba lelele (Mawindoni niko mawindoni)
Simba wa kike hodari katikati ya mawindo Nitatenda kwa akili, kuyafumbua mafumbo Nitanguruma alfajiri, jioni nilete mawindo Sitanyamaza mpaka Mungu anipatie utukufu Simba lelele (Mawindoni niko mawindoni)
I´m a champion (Yeah yeah) Champion (Yeah yeah) Super champion (Oh Yeah yeah) Mimi champion, I´m a winner
I´m a champion (Yeah yeah)
Champion (Yeah yeah) Super champion (Oh Yeah yeah) Mimi champion, I´m a winner
I´m a champion (Yeah yeah) Champion (Yeah yeah) Super champion (Oh Yeah yeah) Mimi champion, I´m a winner