Wanyamazishe bwana Milele wanyamaze Wafunge mpito kwa Yesu Na wakae kimya kimya
Wanyamazishe bwana Wanyamaze Wafunge mpito kwa Yesu Na wakae kimya kabisa
Wapofushe macho yao Wasinione wakae mbali nami Ah wasinione
Kwa kuwa walitangaza msiba juu yangu Wala hawakutaka ipone nafsi yangu Wakafanya sherehe kupitia jina langu Waliona fahari kutangaza mauti yangu Wakachuma na pesa kupitia jina langu Hawakuona vibaya kuumiza familia yangu Walifanya dhihaka kudhihaki watoto wangu
Ah namtuma malaika nyumbani kwao
Atangaze msiba kwenye familia zao Namtuma Gabrieli malangoni kwao Atangaze msiba malangoni kwao
Nawafanye matanga maishani mwao Natangaza msiba kwenye malango yao Natangaza matanga nyumbani kwao Yasikome matanga kwenye familia zao
Laana kifo, iwe juu yao Wala wasiwe salama watoto wao Mauti iwe fungu lao Kushindwa uwe mbele yao Kwa kuwa mimi nimekutumaini