Kama Mungu angechangua watu wake Mimi singekuwepo duniani Kama Mungu angechagua watakatifu Mimi singekuwepo duniani
Mimi binadamu, wala si malaika Mengi nimekosea na kukuchukiza Mi nafanya mambo yasiyo stahili Nimevuruga vuruga mipango yako Wanihurumia Mbele ya macho ya wanadamu Nilikuwa nikijificha Kumbe wewe waniona Kwa kujifanya mtakatifu Tena bingwa mkarimu Nilikuwa/(Kwenye ibada) mnyenyekevu Tena mpole sana Kwa kujifanya mtakatifu Tena bingwa mkarimu Nilikuwa/(Kwenye ibada) mnyenyekevu Tena mpole sana
Sasa nimetambua, mbivu na mbichi ni zipo Sasa ninaelewa, njia salama ni wapi Na nimejua bila ya wewe sifiki Hata nikila pasipo neno lako sishibi Neema yako, ila kwa neema yako Upendo wako, kwa upendo wako Rehema zako zimeniimarisha tena Neema yako, ila kwa neema yako Upendo wako, kwa upendo wako Rehema zako zimeniimarisha tena
Mbele ya macho ya wanadamu Nilikuwa nikijificha Kumbe wewe waniona Kwa kujifanya mtakatifu Tena bingwa mkarimu Nilikuwa/(Kwenye ibada) mnyenyekevu Tena mpole sana Kwa kujifanya mtakatifu Tena bingwa mkarimu Nilikuwa/(Kwenye ibada) mnyenyekevu Tena mpole sana